Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Gen Z Wamshangaza Marioo

Msanii wa Bongo Fleva, Omary Mwanga 'Marioo' ameshangazwa na mapokezi makubwa ya wimbo wake mpya wa OLUWA katika jukwaa la YouTube uliotoka rasmi Desemba 15, 2027.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo ameonesha kukubali nguvu ya mashabiki zake kwa kuufanikisha wimbo huo kufikisha zaidi ya watazamaji zaidi ya 579k YouTube ikiwa ni siku moja tangu video ya wimbo huo kupandishwa kwenye jukwaa hilo.



Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram mkali huyo leo Desemba 16, 2025, amechapisha mfululizo wa picha na kuzisindikiza na maneno yasemayo; Gen Z ni watu na nusu wahenga hawaamini macho yao"

Hii inatokea ikiwa ni siku chache tangu kuanze kwa mjadala unaoonesha mvutano baina ya mashabiki na wasanii wa Bongo Fleva ambapo mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii walitangaza kutowasapoti wasanii katika kazi zao.

Hatahivyo hali imekuwa tofauti kwani katika jukwaa la YouTube wimbo huo umeendelea kusumbua huku komenti kutoka kwa mashabiki wakiendelea kusifia kazi za msanii huyo.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: