Tazama maisha ya nguli wa mzuki wa Hip Hop kutoka Marekani, Diddy akiwa gerezani ambapo anatumikia kifungo katika gereza la ‘Federal Correctional Institution, Fort Dix (FCI Fort Dix)’. Gereza la serikali la shirikisho huko New Jersey, Marekani.
Moja ya video inayosambaa mitandaoni inamuonesha rapa huyo akiwa anafurahia maisha ya gerezani huku baadhi ya wafungwa wenzake wakifichua kuwa Diddy ni mtu tofauti na anayependa kutabasamu kila wakati.
Awali msanii huyo alifungwa katika gereza la Metropolitan Detention Center, Brooklyn ambapo aliwekwa humo tangu kukamatwa kwake Septemba 2024. Lakini baada ya kutokea sintofahamu katika gereza hilo alihamishwa, uhamisho ambao ulifanyika Oktoba 31, 2025.
Utakumbuka Diddy alianza kuhusishwa na kesi mbalimbali mwishoni mwa mwaka 2024 baada ya wanawake kadhaa akiwemo aliyekuwa mpenzi wake Cassie wakishitaki kuteswa na kulazimishwa kuhusika katika biashara za kingono.
Baada ya mashitaka kuwa mengi Polisi wa Marekani walifanya upekuzi katika mijengo yake miwili ukiwemo wa Miami na kukuta vitu mbalimbali ambavyo vilichikuliwa kama ushahidi vitu kama Madawa ya kulevya, bunduki, kanda za video chafu, mafuta ya watoto pamoja na vilainishi zaidi ya 1000.
Chanzo; Mwananchi Scoop