Kutana na Padre Guilherme Peixoto, padre wa Kanisa Katoliki kutoka Ureno ambaye pia ni DJ wa Techno anayetikisa majukwaa makubwa Ulaya.
Kutoka kutoa misa parokiani hadi kuongoza matamasha yenye maelfu ya mashabiki, Padre Guilherme anavunja mipaka na kubadili mtazamo kuhusu imani na muziki.
Kwa midundo mikali ya Techno, anathibitisha kuwa imani na sanaa vinaweza kwenda pamoja, na kwamba ujumbe wa matumaini unaweza kufikishwa kwa njia yoyote hata kupitia muziki wa klabu.
Chanzo; Global Publishers