Mwanamuziki Jason Derulo ameeleza kuwa hatorudia tena kuwa ndani peke yake na mwanamke ambaye anafanya naye kazi baada ya kufunguliwa kesi ya unyanyasaji wa kingono na msanii aliyekuwa akifanya nae kazi (Emaza Dilan).
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ameyasema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo na Bensinger kwenye ‘In Depth With Graham Bensinger’ ambapo amedai kesi hiyo imemgharimu mamilioni ya dola na kupoteza deals kibao, mahusiano na taasisi kubwa na hata kutaka kuiharibu taswira na career yake.
Chanzo; Crown Media