Mwanamuziki Harmonize ameibuka akimjibu Majizzo baada ya kumtaja kuwa msanii aliyetolewa na Diamond Platnumz.
Harmonize amesema, alimwomba Majizzo kutomhusisha Diamond, akidai hitmaker huyo hastahili heshima hiyo ingawa anatambua mchango wake wa awali.
Amesisitiza kuwa ni msanii mkubwa kwa sasa na kwamba Diamond amekuwa akitamani anguko lake, hivyo hawezi kumheshimu.
Pia amemtuhumu kuwa chanzo cha kudorora kwa lebo yake Konde Gang, akisema Diamond aliwapa wasanii wake ahadi hewa.
Harmonize ametaja mfano wa Angella, aliyedaiwa kuahidiwa kolabo na Zuchu ambayo haijatimia, na kudai Diamond alimlipia Ibraah mwanasheria wakati alipotaka kuondoka Konde Gang.
Ametahadharisha kuwa kuanzia sasa atamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayehusisha jina lake na Diamond Platnumz.
Chanzo; Itv