Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Changamoto ya Ubongo wa Kim Kardashian Kumbukumbu

Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu Marekani, Kim Kardashian amegundulika kuwa ubongo wake una uwezo mdogo wa kufanya kazi, uchunguzi ambao umefanywa na daktari bingwa wa afya ya ubongo, Daniel Amen.

Kupitia kipindi kilichooneshwa mwishoni mwa Novemba cha ‘The Kardashians’, Kim alifanyiwa skani ya ubongo akiwa na Scott Disick. Dkt. Amen, ambaye amewahi kuwapima Khloé na Kendall mwaka 2022, alibainisha kuwa sehemu ya mbele ya ubongo wa Kim haifanyi kazi kwa kiwango kinachotakiwa, hali ambayo inaweza kuathiri uwezo wake wa kudhibiti msongo wa mawazo.

Hata hivyo, taarifa njema ni kwamba skani hiyo ilionesha hana hatari kubwa ya kupata Alzheimer’s, wala hana dalili za wasiwasi au mfadhaiko.

Lakini pamoja na hilo, Dkt. Amen alimtaka Kim kuwa makini kutokana na hali hiyo ambayo anadhani huwenda imetokana na msongo wa mawazo wa muda mrefu (chronic stress) unaomkabili Kim kutokana na maandalizi ya mtihani wake wa California bar exam.

Aidha kwa upande wa Kim alisema kuwa anahitaji kupata mpango wa kulitatua hilo sababu ana mambo mengi ya kufanya majira ya kiangazi.

Hata hivyo inaelezwa kuwa msongo wa mawazo kwa Kim hautokani tu na mtihani wake wa sharia lakini unatokana pia na misukosuko aliyoipata wakati wa kudai talaka yake mwaka 2022 kutoka kwa aliyekuwa mume wake Kanye West (Ye).

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: