Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

WCB Mabegani Mwa Zuchu, D Voice

Kwa mara nyingine tena D Voice na Zuchu wanaonyesha kwa nini wanastahili kuwepo WCB Wasafi kwa jinsi wanavyoipambania chapa hiyo kupitia mfululizo wa muziki mzuri kutokea kwao.

Ukimtoa Diamond Platnumz kama mwanzilishi na mmiliki wa WCB Wasafi, Zuchu na D Voice ndio wasanii pekee waliosalia katika lebo hiyo ambayo ilianzia kuwatoa wanamuziki zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Hivi karibuni D Voice na Zuchu wameachia wimbo wao mpya, Baridi (2026) uliotayarishwa na Trone ambaye amewahi kuhusika katika nyimbo za Zuchu kama Sukari (2021), Utaniua (2023), Wale Wale (2024) n.k.

Baridi ni wimbo wa mapenzi uliojaa hisia, mvuto na simulizi ya uhusiano uliopamba moto, huku ukinogeshwa na midundo laini na maneno yanayogusa moyo ambayo yanaendana na wanaopenda nyimbo za mapenzi.

Kupitia Baridi, wasanii wote wawili kwa kiasi kikubwa wameonyesha uwezo wa kuzitumia vizuri sauti zao kwa lengo la kuburudisha, sauti ambazo zimepambwa na uandaaji nzuri na wa kisasa wa muziki.

Ndani ya muda mfupi wimbo huo umepata mapokezi mazuri hasa katika majukwaa ya kidijitali ya kusikiliza muziki na ndipo hasa wasanii wengi wameelekeza nguvu kubwa maana soko lenyewe ndiyo hilo.

Tayari umeshika namba moja katika mitandao ya YouTube, Boomplay, Audiomack na Shazam kwa upande wa Tanzania, na unatazamiwa kufika mbali zaidi kimauzo (streams) katika majukwaa mengine.

Ikumbukwe hao ndio wasanii wa mwisho kusainiwa na kutambulishwa WCB Wasafi na Zuchu alitoka mwaka 2020 kupitia Extended Playlist (EP) yake ‘I Am Zuchu’ ambayo ilibeba wimbo maarufu ‘Wana’ uliomtambulisha vizuri.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: