Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Miaka 12 ya Kifo cha Poul Walker

Novemba 30, 2013, dunia iligubikwa na simanzi baada ya kumpoteza mwigizaji wa filamu nchini Marekani, Paul Walker, ambaye kwasasa ametimiza miaka 12 tangu afariki dunia baada ya kupata ajari ya gari huko Valencia, Santa Clarita, California, United States.

Kulingana na ushahidi wa kitaalamu uliokusanywa kutoka eneo la tukio, mwigizaji huyo hakuwa pekeyake kwenye gari. Rodas alifariki papo hapo kutokana na majeraha mengi ya kimwili, wakati Walker alifariki ndani ya sekunde chache kutokana na athari za pamoja za majeraha ya kimwili na majeraha ya moto. Miili yao yote miwili iliungua kiasi cha kutoweza kutambulika.

Paul Walker alifahamika zaidi kwa uhusika wake katika filamu ya 'Fast & Furious', akifahamika kama Brian O'Conner. Alifariki kabla ya kumaliza kurekodi filamu ya ‘Furious 7’.

Kaka zake Caleb na Cody Walker waliingia ili kukamilisha filamu hiyo huku wimbo maarufu wa 'See You Again' wa Wiz Khalifa na Charlie Puth ukitengenezwa kama zawadi kwa muigizaji huyo.

Moja ya matukio ya mwisho katika 'Fast Furious 7' linaonyesha Brian (Paul Waker) na Dominic Toretto (Vin Diesel) wakiendesha gari pamoja mara ya mwisho kabla ya njia zao kutofautiana kama inavyoonekana katika wimbo wa 'See You Again' wa Wiz Khalifa na Charlie Puth.

Uhusika wake unasalia hai ndani ya ulimwengu wa Fast & Furious, huku akitajwa mara kwa mara nje ya filamu hiyo na mara nyingine picha zake huonekana kwenye kumbukumbu katika filamu zijazo kama Fast X.

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuhusiana na mada hii: