Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kuhusu P Diddy Kuhusika na Mauaji ya 2pac na Biggie

Documentary mpya ya 50 Cent “Sean Combs: The Reckoning” iliyotua Netflix imeibua madai mazito kuhusu Sean “Diddy” Combs ikichora safari yake ya kupanda na kuanguka kwa mtikisiko mkubwa.

Katika sehemu ya pili, wafanyakazi wa zamani wa Bad Boy Records na wasanii kama Mark Curry wanaeleza kwa mara ya kwanza kile walichokiona nyuma ya pazia kuhusu mauaji ya Biggie Smalls na Tupac Shakur. Wanadai Diddy alikuwa na ushiriki wa kina, na kwamba alichochea chuki ya Mashariki na Magharibi iliyolitikisa hip-hop miaka ya ’90.

Kirk Burrowes, mwanzilishi mwenza wa Bad Boy, anadai Diddy alimlazimisha kumkabidhi hisa zake akimtishia kwa pinde la baseball, na kwamba “Diddy alimwonea wivu Biggie na wengine kwa kipaji chao.”

Kwa upande wao, timu ya Diddy imetaja documentary hiyo kama “hit piece yenye upendeleo”, wakisema madai hayo hayana ushahidi na yametolewa na watu wenye kinyongo cha zamani.

Lakini madai yanazidi kushika moto hasa baada ya kutajwa kwa taarifa za mahakamani kuwa Diddy aliwahi kutuhumiwa kuweka dau la dola milioni moja kwa vichwa vya Tupac na Suge Knight, madai ambayo ameyakana.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: