MSANII anayefanya vizuri katika tamthilia ya Kombolea, Farid Mohammed ‘Cholo Kobis’ amesema tamthilia hiyo imemtambulisha kwa jamii, lakini anachukiwa na baadhi ya wazazi wasiofahamu ni maigizo tu.
Cholo ambaye ameigiza kama kibaka au mtukutu kwenye tamthilia hiyo, amesema kwenye maisha yake ya uhalisia ni mtu wa ibada sana, lakini hakuna mtu anaweza kuelewa kutokana na kazi anayoifan-ya.
“Maisha yangu binafsi na Kombolela ni vitu viwili tofauti, lakini licha ya yote anayoyapitia hasa kwenye kuchukiwa anajivunia kwani anaamini anachokifanya kinaifikia jamii vizuri na wanakielewa,” amesema na kuongeza, siku ya kwanza wanamwambia anatakiwa kuigiza aina ya maisha hayo alikuwa tayari amepata picha ya kuna mashabiki watakaomkubali na watakaomchukia.
Akizungumzia tamthilia hiyo kwa jumla, amesema imempa jina kubwa na kazi zaidi, huku akiwataka waandaaji kumpigia simu kwani bado anataka mafanikio zaidi.”
Chanzo; Mwanaspoti