Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chuando Mzee Mwenye Muonekano wa Kijana Anayeshangaza Wengi

Mfahamu Chuando Tan mwanamitindo na mpiga picha kutoka Singapore ambaye ameendelea kuwashangaza wengi kutokana na muonekano wake kama kijana licha ya kuwa na umri mkubwa.

Chuando Tan alizaliwa mwaka 1966 nchini Singapore. Hata hivyo, mtu akimuona kwa mara ya kwanza hudhani ni kijana wa miaka 20 au 30. Hali hiyo imewafanya watu wengi duniani kushangaa na kujiuliza siri ya mwonekano wake wa ujana unaozidi kadiri miaka inavyosonga.

Kabla ya kuwa mpiga picha maarufu, Chuando Tan aliwahi kuwa mwimbaji wa muziki wa pop katika miaka ya 1990. Baada ya muda, alibadili mwelekeo wa kazi yake na kuingia katika ulimwengu wa upigaji picha za mitindo. Kipaji chake kilianza kung’ara haraka, na baadaye akawa mmoja wa wapiga picha wanaoheshimika katika tasnia ya mitindo barani Asia.

Mbali na upigaji picha, Chuando Tan pia amejipatia umaarufu mkubwa kama mwanamitindo. Mwili wake unaoonekana kijana umevutia maelfu ya watu wanaofuatilia maisha yake. Umaarufu wake uliongezeka zaidi baada ya kuanza kushiriki picha zake katika mtandao wa Instagram, ambapo ana mamilioni ya wafuasi wanaovutiwa na maisha yake ya mazoezi, mitindo.

Kwa mujibu wa Chuando Tan mwenyewe, siri ya kuendelea kuonekana kijana ni nidhamu katika maisha ya kila siku. Anasema hufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara, hasa mazoezi ya kujenga misuli na kujiweka katika hali nzuri ya afya. Pia hujali sana lishe yake kwa kula chakula chenye virutubisho na kuepuka vyakula vinavyoweza kudhoofisha afya.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: