Katika juhudi za kuenzi urithi wa Mtwa Mkwawa kama shujaa wa kihistoria na mwanzilishi wa Uhehe wa sasa, Chifu wa Wahehe, Mtwa Adam Sapi II, ametangaza mpango wa kutengenezwa kwa filamu maalum itakayohusu maisha na ushujaa wa Chifu Mkwawa. Filamu hiyo inalenga kuonesha historia, mapambano na mchango wa Mtwa Mkwawa katika kulinda utamaduni wa Wahehe pamoja na kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumza na Crown TV, Mtwa Adam Sapi II amesema filamu hiyo itakuwa nyenzo muhimu ya kuelimu na kitamaduni, itakayosaidia vizazi vya sasa na vijavyo kuifahamu historia ya kweli ya Mtwa Mkwawa na thamani ya utamaduni wa Kihehe.
Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Mkwawa Foundation, watahakikisha filamu hiyo inatengenezwa kwa ubora wa kimataifa na kusambazwa ndani na nje ya nchi, ili kukuza utalii wa utamaduni na kuifanya historia ya Wahehe kuwa sehemu ya maudhui yanayotambulika duniani.
Chanzo; Crown Media