DJ maarufu wa redio na klabu za muziki nchini Afrika Kusini, Warrick Stock maarufu kama DJ Warras, amepigwa risasi na kuuwawa katikati ya Johannesburg siku ya jana Desemba 16, Polisi wamesema alishambuliwa na washukiwa watatu baada ya kuegesha gari lake, mmoja alimpiga risasi kabla ya kukimbia.
Warras alikuwa mtangazaji maarufu wa redio, televisheni, na podikasti, siku ya Jumanne Desemba 16, nje ya Zambezi House alipokuwa akiangalia ufungaji wa mifumo ya usalama karibu na Carlton Centre,Polisi wanaendelea kuchunguza tukio hili na kutafuta washukiwa kupitia video za CCT.
Chanzo; Bongo 5