Simu ya mkononi imekuwa sehemu muhimu ya mawasiliano yetu kila siku. Lakini sasa, kifaa hiki ndicho kinachotajwa kama sababu kubwa na rahisi zaidi ya kuvunjika kwa ndoa na mahusiano.
Tafiti zinaonyesha kwamba kiasi cha talaka kinaongezeka kila uchao, hasa kwa watu wa umri wa makamo na mara nyingi chanzo ni kilekile: simu ya mwenza. Kilichoanza kama chombo cha faraja na kuwaleta watu karibu, kwa wengine kimegeuka kuwa sumu ndani ya ndoa.
Chanzo; Bbc