Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Jinsi ya Kuiwekea Simu Yako Ulinzi Salama

Kwenye ulimwengu wa kidijitali wenye mabadiliko ya kasi, yawezekana simu yako imekuwa moja ya maitaji muhimu kwenye maisha yako hasa katika kuhakikisha shughuli zako za kimawasiliano zinasonga. Pia ni kifungashio cha hadhina zako muhimu yakiwemo mambo binafsi, picha za familia, mazungumzo ya siri, na hata maelezo ya benki. 

Hivyo, bila ulinzi wa kutosha, unaweza kupoteza yote haya kwa urahisi au kuwa muhanga wa wizi wa kidijitali, bila kujihami unaweza kujikuta umepoteza vitu vyako vya msingi, anaitwa Fernando Corbató – ambaye alibadilisha historia ya usalama wa kompyuta.

Fernando José Corbató alizaliwa 1926 California, Marekani. Alikuwa mwanasayansi hodari wa kompyuta na profesa katika Chuo Kikuu cha MIT. Alipata shahada yake ya uzamili na kuanza kufanya utafiti wa mifumo ya kompyuta ambayo ingekuwa na athari kubwa kwa vizazi vijavyo. “

1961, Corbató akifanya kazi kwenye mradi wa Compatible Time-Sharing System, au CTSS. Hii ilikuwa mojawapo ya mifumo ya kwanza ya kompyuta inayoruhusu watumiaji wengi kushiriki kompyuta moja kwa wakati mmoja. Kabla ya hapo, kompyuta ilikuwa ikitumika na mtu mmoja tu kwa wakati mmoja, lakini Corbató alitaka kubadilisha hilo.

Wakati watumiaji wengi walipoanza kushiriki kompyuta moja, tatizo kubwa liliibuka. Je, watumiaji wangewezaje kulinda faili zao binafsi ? Je, mtu mmoja angeweza kuingia kwenye faili za mwingine bila idhini? Hapa ndipo Corbató alipopata wazo. Aliamua kuunda njia ya kuthibitisha utambulisho wa kila mtumiaji kabla ya kutoa ufikiaji.

Corbató aliunda wazo la nywila maarufu “Password” neno la siri ambalo mtumiaji pekee ndiye anajua. Nywila hii ilihitajika kila wakati mtumiaji anapotaka kuingia kwenye akaunti yake. Hii ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya kompyuta ambapo ulinzi wa data ulianza kutumia nywila. Ugunduzi huu ulikuwa msingi wa usalama wa kisasa wa kidijitali.

Ugunduzi wa Corbató haukuishia hapo. Aliendelea kufanya kazi na mifumo mingine kama UNIX, ambayo bado inatumika hadi leo katika simu na kompyuta nyingi. Nywila ilianza kutumika kila mahali – kutoka benki hadi mitandao ya kijamii. Hadi leo, mabilioni ya watu duniani wanategemea nywila kulinda maisha yao ya kidijitali.

Licha ya Corbató kufariki dunia Julai,12,2019 alifanikisha kuiachia dunia ya kidijitali urithi wake ambao unaendelea kuishi. Ambopo huwenda umemshukuru mara kadhaa kwa jinsi password zilivyokuokoa kwenye mabo yako kadhaa 

Kwanini historia ya Corbató, ni kujua usalama wa simu yako ulikotokea, hizi hapa ni njia kadhaa za jinsi ya kutumia kanuni zake  kulinda simu yako kwa njia ya password…

Kwanza, anza na nywila imara. Epuka kutumia nywila rahisi kama nambari za mfululizo yani 123456 au jina lako la mwisho. Badala yake, tumia mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo, nambari, na alama za kikomo. Nywila kama hiyo ni ngumu kudhaniwa na huzuia wavamizi wa kidijitali.

Pili, tumia uwezo wa biometric wa simu yako. Simu nyingi za kisasa zina skana ya vidole au utambuzi wa uso “Faceid”. Hii inakuwezesha kufungua simu kwa kugusa kidole au kuangalia kamera. Ni haraka, rahisi, na salama zaidi kuliko nywila pekee.

Tatu, sasisha mfumo wako wa uendeshaji mara kwa mara. Kila sasisho huja na marekebisho ya mapungufu ya usalama. Usipuuze notifikesheni za sasisho, zifungue mara moja. Hii inazuia wadukuzi kutumia mapungufu ya zamani kuingia kwenye simu yako.

Nne, washa uthibitisho wa hatua mbili, au 2FA, kwenye akaunti zako zote muhimu. Hii inamaanisha hata kama mtu anapata nywila yako, bado anahitaji simu yako au programu nyingine ili kuthibitisha uingiaji. Ni kinga ya ziada ambayo inafaa sana kwa benki na barua pepe.

Tano, epuka kutumia Wi-Fi za umma bila VPN. Mitandao ya umma mara nyingi hayana ulinzi wa kutosha, na wadukuzi wanaweza kuiba data yako. Tumia VPN ili kuficha shughuli zako za mtandao. Hii inafanya data yako iwe salama hata kwenye mtandao usio salama.

Sita, weka programu ya kingavirus kwenye simu yako. Kuna programu nyingi za kuaminika kama Avast au Malwarebytes zinazochanganua simu yako mara kwa mara. Zinaweza kugundua na kuondoa virusi au programu hasidi kabla hazijaharibu data yako.

Saba, tumia kipengele cha kupata simu yako ikiwa itapotea. Kwenye Android, nenda kwenye tovuti ya Google na utafute simu yako. Kwenye iPhone, tumia iCloud. Unaweza kuifunga au kuifuta data kwa mbali ikiwa itaibiwa.

Nane, zuia programu zisizojulikana kuingia kwenye simu yako. Kwenye Android, zima chaguo la kusakinisha programu kutoka vyanzo visivyojulikana. Hii inazuia programu hasidi kuingia bila idhini yako.

Tisa, futa data za zamani mara kwa mara. Cache, historia ya tovuti, na faili zisizohitajika zinaweza kuwa hatari ikiwa zitaanguka mikononi mwa wadukuzi. Tumia zana za simu yako kufuta data hizi kwa urahisi.

Kumi, weka nakala za data yako kwenye wingu. Tumia Google Drive au iCloud kuhifadhi picha, video, na hati zako. Hii inakusaidia kupata data yako hata kama simu itaharibika au kupotea.

Kumi na moja, usibonye linki za ajabu kwenye SMS au WhatsApp. Hizi mara nyingi ni mtego wa wizi wa data. Ikiwa una shaka, uliza au tafuta habari kwenye tovuti rasmi kabla ya kubonyeza.

Kumi na mbili, weka screen lock iwashwe moja kwa moja baada ya dakika moja. Hii inazuia mtu yeyote kuingia kwenye simu yako ikiwa utaiacha wazi kwa bahati mbaya.

Kumi na tatu, tumia programu ya kusimamia nywila. Programu kama LastPass au Bitwarden zinakusaidia kuunda na kuhifadhi nywila ngumu bila kuzikumbuka zote. Hii inafanya maisha yako yawe rahisi na salama.

Kumi na nne, jifunze kuhusu hila za wadukuzi. Wengi hutumia mbinu za kijamii kama phishing ili kukudanganya. Kuwa makini na ombi lolote la nywila au maelezo ya benki.

Kumi na tano, linda watoto wako kwenye mtandao. Tumia mipangilio ya mzazi kwenye simu au programu ili kuzuia maudhui hatari. Hii inawakinga na wanyama wa mtandaoni.

Kwa kumalizia, ulinzi wa simu yako sio kazi ya siku moja. Ni mazoea ya kila siku yanayohitaji wa kila siku.

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: