Wachina wamezua balaa mitandaoni baada ya kuzindua application mpya ya kufuatilia usalama wa watu ijulikanayo kama Demumu au ‘Are You Dead’.
App hii imebuniwa mahsusi kwa ajili ya watu wanaoishi peke yao majumbani, iwe ni mijini au vijijini, ili kusaidia kuthibitisha kama bado wako hai au la.
Kupitia mfumo wake rahisi, mtumiaji anatakiwa kutoa uthibitisho wa mara kwa mara kwamba yuko salama, na endapo hilo halitafanyika kwa muda uliopangwa, tahadhari hutumwa kwa ndugu au wahusika waliowekwa.
Umaarufu wa app hii umeongezeka kwa kasi baada ya watu wengi kuona faida yake katika kupunguza vifo visivyofahamika, hasa kwa wazee au watu wanaoishi bila mtu wa karibu.
Wadau wa teknolojia wanaiona kama hatua muhimu katika matumizi ya teknolojia kwa ustawi wa jamii, huku wengine wakijadili masuala ya faragha. Hata hivyo, ‘Are You Dead’ imeonekana kuwa suluhisho la kipekee katika kulinda maisha ya watu wanaoishi pekee yao.
Chanzo; Mwananchi Scoop