Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

VPN Inavyofanya Kazi na Jinsi Inavyoweza Kukuingiza Mkenge

Watu wengi wanauliza kuhusu Matumizi ya VPN na Ufahamu iwapo SERIKALI na Mtoa huduma wako wanajua kwamba unatumia VPN.  Tukitaka kuongelea VPN inabidi tuanzie mbali ili kuelewa nini haswa tunaongelea na umuhimu wake. Hii itatusaidia kupata uelewa na elimu pana.  

VPN kwa kirefu ni Virtual Private Network. Yani ni server binafsi ambayo inakupa uwezo wa kupata huduma ya internet huku ikificha/kuweka siri nini haswa unafanya mtandaoni.  

Lakini nikisema hivyo huenda bado kuna mtu nimemuacha. Tuanzie nyuma kidogo kwenye maana ya INTERNET.  

Mwanzo njia ya taarifa ilikuwa hivi  

KWAKO -> ISP -> KWANGU  

Alafu inaanza kurudi  

KWANGU -> ISP -> KWAKO  Select an option

Na hapo ISP anaona kila kitu unachofanya. Lengo la VPN sasa kumficha ISP asijue nini unafanya. Hilo ndilo lengo kubwa ukiacha pia kuficha location yako kwamba uko wapi.  

Sasa VPN inachofanya ni inapochukua taarifa kutoka kwako inazipiga encryption ili mtu akizipata asiweze kuzifungua. Ufunguo wa hizi taarifa uko kwako na kwa VPN server.  

Lakini pia inaficha IP address unayotaka kufikia ndani ya hiyo data packet. Haijamuondoa ISP hapo kati.  

Ruti ya taarifa yako sasa hivi inabadilika.  Taarifa inapotoka kwako imeshapigwa encryption na ile VPN service uliyoweka, Ikitoka kwako inaenda kwenye server za ISP wako.  

Sasa hivi ISP anaona umetuma request kutoka kwako kwenda kwenye ile ISP server tofauti na mwanzo. Kwahiyo wewe unataka kufikia http://habaritechtz.com bila ISP wako kujua si ndiyo?  VPN imechukua hiyo request na kuficha yaliyomo ndani.  

Hiyo request ikifika kwenye VPN server inakuwa decrypted na inaenda mahali husika , Habaritech inarudisha taarifa kwenye VPN server  

Taarifa inapigwa tena mficho madhubuti kabisa ndio inarudishwa kwa ISP. ISP anachojua taarifa imeenda kwenye VPN na VPN imerudisha majibu. Majibu yakifika kwako yanakuwa decrypted/kufunguliwa na wewe unasoma ukiwa na raha kabisa. ISP anakuwa haoni kile unawasiliana au kuperuzi lakini si kila VPN inaulinzi huo, tunashauriwa kutumia "VPN with obfuscation technology"  

Hivyo ndivyo VPN inafanya kazi na unaweza kubadili hata location ya IP address yako (mahala ulipwakapewa. Kwahiyo ulichofanya inakuwa hakuna.  

Unapochagua VPN chagua ile ambayo haifanya information loggingo) na pia kupata huduma ambazo huwezi kupata bila VPN pia kuficha content za mawasiliano yako.  

Ila hizi VPN pia ziko na shida. VPN ambazo zinafanya information logging kama ISP.  Hizi nazo ni za kuziepuka maana Serikali inaweza kwenda na court order kuomba hizo taarifa na  na wana strict protocol za encryption ambazo hata wao hawatoona unachofanya.  

Mfano wa hizo VPN ziko nyingi kama Express VPN, Nord VPN, Proton VPN, Surfshark etc.. (zile za kulipia)  

VPN ni zana muhimu ya kuhifadhi faragha yako mtandaoni, hasa katika nchi kama yetu ambapo kuna vizuizi vya mtandao. Lakini chagua vizuri ili usiweke data yako hatarini. Kama una masuala zaidi, jaribu VPN za kulipia na obfuscation ili kuepuka kufungwa.  

Chanzo: TOT Techs

Kuhusiana na mada hii: