Google imeanza Desemba kwa kufanya maboresho muhimu ndani ya toleo jipya la Android 16 QPR2, yakilenga kuongeza usalama, kasi na matumizi bora ya mfumo kwa watumiaji wa simu za Android. Maboresho hayo yanatajwa kuboresha utendaji wa mfumo mzima, kufanya simu kufanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi hata kwa watumiaji wa kawaida.
Kupitia sehemu ya usalama, Google imeongeza ulinzi madhubuti dhidi ya vitisho vya kimtandao, hatua inayolenga kuhakikisha vifaa vya Android vinabaki salama bila kujali mazingira ya matumizi. Aidha, programu ya Health Connect imeboreshwa zaidi na sasa inaweza kufuatilia na kuhifadhi taarifa za kila hatua unayochukua, pamoja na viashiria vingine muhimu vya afya vinavyochangia ustawi wa mtumiaji..
Chanzo; Mwananchi Scoop