Katika ulimwengu wa teknolojia, jina la Elon Musk limekuwa ishara ya misukumo mipya, uvunjaji wa mipaka, na ubunifu unaotangulia wakati.
Kutoka roketi zinazotumika zaidi ya mara moja za SpaceX, magari ya umeme ya Tesla, hadi miradi ya akili bandia na Neuralink, Musk ameandika sura mpya katika sayansi ya kisasa.
Sasa, taarifa nyingine zinazovuma zinasema kuwa anaandaa hatua nyingine kubwa: uzinduzi wa simu mpya inayoitwa Tesla Pi Phone.
Lakini nini hasa kinachofanya uvumbuzi huu kuwa tofauti? Na kwa nini ulimwengu mzima wa teknolojia umeanza kutazama kwa makini?
Simu yenye Muunganisho wa Moja kwa Moja na Starlink
Kipengele kikubwa kinacholeta msisimko ni kwamba Tesla Pi Phone inatarajiwa kutumia mtandao wa moja kwa moja kutoka kwa satelaiti za Starlink ambayo ni teknolojia inayomilikiwa na SpaceX.
Hii ina maana kuwa simu inaweza kufanya kazi maeneo yote duniani, iwe jangwani, baharini, milimani, maporini au maeneo yasiyo na minara ya simu
Kwa mara ya kwanza, mtu anaweza kupiga simu, kutuma ujumbe, au kutumia intaneti maeneo ambayo leo hii yanachukuliwa kuwa “nje ya mtandao.”
Kuchaji kwa Nishati ya Jua – Hatua ya Kuokoa Betri
Elon Musk tayari anamiliki kampuni kubwa ya nishati safi: SolarCity.
Kwa hivyo haishangazi kwamba tetesi zinaonesha kuwa Tesla Pi Phone itakuwa na paneli ndogo za sola zinazowezesha betri kujichaji jua linapopatikana.
Hii inaweza kuwa suluhisho muhimu kwa watu wanaosafiri mara nyingi, wanaoishi maeneo yenye umeme usioaminika, au wanaopenda teknolojia isiyohitaji utegemezi wa soketi kila mara.
Chanzo; Global Publishers