Kim Kardashian amefichua kuwa alitumia ChatGPT kujisomea kwa ajili ya mitihani yake alipokuwa chuoni akisomea sheria. Kim alitoa kauli hiyo alipokuwa na mwigizaji mwenzake wa All’s Fair, Teyana Taylor, wakati wa mahojiano yao ya tarehe 3 Novemba kwenye kipindi cha Vanity Fair’s Lie Detector Test.
Kim alisema:
“Nilikuwa natumia kwa ushauri wa kisheria. Kwa mfano, nikihitaji kujua jibu la swali, nilikuwa napiga picha na kuiweka humo ndani. Lakini mara nyingi majibu yake huwa si sahihi. Imenifanya nifeli mitihani. Halafu ninakuwa na hasira, namkemea kama, ‘Umenifeli! Kwa nini umefanya hivi?’”
Hivi karibuni, kampuni ya OpenAI imetangaza kuwa ChatGPT haitaruhusiwa tena kutoa ushauri wa kisheria au kiafya.
Chanzo; Bongo 5