Program ya ChatGPT imeingia kwenye rekodi ya kuwa program iliyoongoza kupakuliwa zaidi (download) duniani ndani ya mwaka huu wa 2025 ikiwa programu ya bure iliyopakuliwa zaidi, ikiongoza orodha ya App Store mbele ya Google, TikTok, WhatsApp na Instagram.
Orodha ya mwisho wa mwaka inaonyesha kuwa akili bandia (AI) na majukwaa ya kijamii yanaongoza mienendo ya watumiaji, huku ChatGPT ikiipita programu zilizokuwepo kwa muda mrefu, na Threads ikionyesha kuendelea kwa hamasa ya miundo mipya ya mitandao ya kijamii inayohusiana na mifumo iliyopo.
Kwa ujumla, viwango hivi vinaakisi mabadiliko mapana kuelekea zana za vitendo zinazoendeshwa na AI kuwa sehemu ya matumizi ya kila siku, sambamba na burudani na mawasiliano ya kawaida.
ChatGPT ilianza kutumika rasmi tarehe 30 Novemba 2022.
Siku hiyo OpenAI iliitoa kwa umma kwa mara ya kwanza kama toleo la majaribio (public release), na tangu hapo imeendelea kuboreshwa na kupanuliwa hadi kufikia matumizi ya sasa.
Chanzo; Bongo 5