Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tume Yabaini Tozo Mpya Mwiba Hatari kwa Biashara

Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi Nchini, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amesema Tume hiyo imebaini viwango vikubwa vya baadhi ya kodi na uanzishwaji wa tozo, kodi, ushuru, ada mpya bila kuzingatia vya kutosha malengo mengine ya kitaifa hivyo kuleta vilio kwa Walipa kodi lakini pia Tume imebaini
mfumo wa utatuzi wa migogoro ya kikodi bado Wadau hawaridhiki nao.

Akiongea leo March 18,2026 Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa kuwasilisha ripoti ya Tume hiyo kwa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Sefue amesema “Lengo la mapendekezo ya Tume ni kuhakikisha kodi zisiwe kikwazo dhidi ya vita ya umasikini, Tume imebaini viwango vikubwa vya baadhi ya kodi na uanzishwaji wa tozo, kodi, ushuru, ada mpya bila kuzingatia vya kutosha malengo mengine ya Kitaifa na hii huleta hali ya kutotabirika na kuathirika uwekezaji na biashara”

“Tume imebaini mfumo wa utatuzi wa migogoro ya kikodi bado Wadau wanaona hauridhishi na walipa kodi wana mashaka na wana poteza imani na mfumo uliopo wakiona vyombo vya utatuzi wa migogoro havina uhuru wa kutosha kimfumo na kiutendaji”

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: