Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwarobani Haki, Usawa Ulipaji Kodi Kunyweka Hivi Karibuni

Kilio cha baadhi ya wafanyabiashara kuhusu mfumo wa haki na usawa katika ulipaji wa kodi kinakwenda kupata muarobaini, baada ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi kutoa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano, Machi 18, 2026 wakati Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi nchini, katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais Samia amesema:

“Ndugu zangu nimesikiliza kwa makini mapendekezo yaliyotolewa na Tume, ambapo pamoja na mambo mengine yanajielekeza kuboresha sera na sheria za kodi, mazingira ya uwekezaji na biashara, mifumo ya Tehama, kitaasisi ya ukusanyaji mapato na maduhuli na utatuzi wa migogoro ya kikodi.

Kwa ujumla tukiyatekeleza vyema, mapendekezo yaliyotolewa yatatuelekeza katika mfumo wa haki na usawa katika ulipaji wa kodi. Kuna malalamiko mengi, kuna wengine wanalipa sawa, wengine wana vichochoro vya kupita na kulipa kodi kidogo.

Rais Samia ameongeza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanapitisha bidhaa kwa magendo na kusababisha uwanja wa soko kutokuwa sawa, hivyo mapendekezo ya Tume yanalenga kuhakikisha kodi inatozwa kwa haki na usawa kwa kila mfanyabiashara kulingana na kiwango cha biashara anayoifanya.

Tume ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi ilianzishwa Oktoba 4, 2024, baada ya zaidi ya miaka 30 tangu kuundwa kwa tume kama hiyo na Edwini Mtei (marehemu).

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: