Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waliojiajiri Kuanza Kunufaika na Pensheni Uzeeni

Wananchi waliojiajiri sasa wanaweza kunufaika na mafao ya pensheni ya uzeeni,urithi,ulemavu,uzazi, matibabu pamoja na mafao mengine ambayo awali hayakuwa yakipatikana kwa kundi hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amesema hakuna sababu kwa mwananchi aliyejiajiri kushindwa kujiunga na mfuko huo kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa ambayo yanawawezesha kunufaika na mafao mbalimbali sawa na waajiriwa wa sekta ya umma na binafsi.

Mshomba alitoa kauli hiyo wakati alipowaongoza wafanyakazi wa NSSF kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na kuandikisha wanachama wapya katika soko la Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, kupitia kampeni ya NSSF Staa wa Mchezo Paka Rangi.

Alisema mwananchi atakayejiajiri na kujiunga na NSSF atanufaika na mafao ya pensheni ya uzeeni, urithi, ulemavu, uzazi, matibabu pamoja na mafao mengine ambayo awali hayakuwa yakipatikana kwa kundi hilo.

“Tunaposema wanachama wa NSSF ni mastaa wa mchezo, tunamaanisha kuwa mfuko unatoa uhakika wa maisha bora, matibabu na kipato hata pale mwanachama anapostaafu. Endapo mwanachama atafariki, wategemezi wake watanufaika na mafao ya urithi,” alisema Mshomba.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: