Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bandari Yakodishwa kwa Dp World Haijauzwa, Serikali Yasisitiza

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, ameendelea kusisitiza kuwa Bandari ya Dar es salaam haijauzwa bali imepangishwa kwa DP World na Wawekezaji wengine ili kuiendesha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Msigwa amesema “Mamlaka ya Bandari Tanzania kama wote mnavyojua na kama ambavyo nilisema uamuzi makini uliofanywa na Mh. Rais iliingia mkataba wa upangishaji na uendeshaji Bandari, na naomba nipigie mstari hii tuliingia mkataba wa upangishaji na uendeshaji maana yake wapo baadhi ya Watu wanapotosha wanaenda kusema Bandari ya Dar es salaam imeuzwa, Bandari haijauzwa ni mali ya Serikali, DP World na Adan tumeingia nao mkataba wa uendeshaji”

Msigwa amesema DP World tangu iingie mkataba wa upangishaji na uendeshaji wamewekeza bilioni 214.2 na kuboresha Bandari hiyo ikiwemo kuongeza mitambo na kufanya sasa Bandari kutoa huduma bora zaidi.

Msemaji Mkuu amesema Bandari imetoa zaidi ya ajira 700 na mizigo sasa inahudumiwa kwa siku 6 tu kutoka siku 30 za hapo awali huku ongezeko la shehena kufikia tani milioni 27.7 sawa na asilimia 17 na Bandari sasa ikiongeza mapato na TPA na TRA hadi kufikia trilioni 2 kwa mwezi.

 

 

 

Chanzo; Milllard Ayo

Kuhusiana na mada hii: