Kufuatia vurugu zilizofanyika siku ya Uchaguzi Mkuu 2025, Oktoba 29 zilizosababisha majanga kadhaa ikiwemo kibiashara na hata kiuchumi, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Albert Chalamila aja na suluhisho kwa wote waliopoteza mizigo iliyokuwa ikisafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine siku ile.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Novemba 7,2025 ameweka wazi utaratibu wa namna muhusika anaweza kuupata mzigo wake.
“Polisi na vyombo dola ambavyo vimekuwa barabarani siku ya tarehe 29, yapo magari yaliyobeba mizigo ya mafuta na mizigo mingne yapo magari yaliyounguzwa kichwa lakini mzigo haukuungua.
“kwenye baadhi ya magari tulitoa barabarani mizigo na kuiweka eneo maalumu, tumeweka utaratibu kwa kusaidiana na TRA, Ewura na Jeshi Polisi kwa wale wanaodhani mizigo inawahusu watakuwa na vibali vyote vinavyohusu umiliki baada ya kujilidhisha atakabidhiwa mzigo.” Albert Chalamila
Chanzo; Tanzania Journal