Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mfumo Mpya wa TRA Mabambikizo ya Kodi Kukomeshwa

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, ameendelea kusisitiza kuwa Bandari ya Dar es salaam haijauzwa bali imepangishwa kwa DP World na Wawekezaji wengine ili kuiendesha.

Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Msigwa amesema “Serikali kupitia TRA pamoja na kuongeza ukusanyaji mapato baada ya kutumia njia za kisasa na kitaalamu, imeamua kuwekeza Tsh. bilioni 100 kuweka mfumo ambao utakuwa rafiki kwa Walipa kodi wote kulipa kodi”

“Yale mambo ya kukutana na Watu na wengine wanakuwa sio Waadilifu wanakuletea hesabu ambazo hazieleweki, sasa tunakwenda kuwekeza kwenye mfumo ambao Mlipa kodi ataweka na kufuatilia hesabu zake na kujua analipa nini kilicho halali Serikalini”

“Mfumo huu tunauzindua February 09, Wafanyabiashara tuupokee kwa mikono miwili , ni mfumo mzuri na ndiko Dunia ilipo sasa, mambo ya kukadiriana hesabu kwa peni na kuminyaminya calculator huku tunaangaliana usoni huyu Msigwa nimkomeshe, huyu alinikwaza sehemu fulani nimfanyie hivi, sasa ni mfumo hakuna kuonewa kila Mtu atalipa kodi kwa usawa”

 

 

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: