Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ujumbe wa Lissu Kusomwa Kumbukizi ya Mzee Mtei

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Tundu Lissu, aliyeko Gereza la Ukonga kutokana na kesi inayomkabili ya uhaini, anatarajiwa kutuma ujumbe maalumu unaomhusu mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei.

Ujumbe huo unatarajiwa kwenda kuchukuliwa leo ambao utasomwa katika kumbukizi ya Mzee Mtei itakayofanyika Januari 23, 2026 kabla ya maziko yake yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Januari 24, 2026 nyumbani kwake Tengeru, Arusha.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Januari 21, 2026 na Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, Amani Golugwa, akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa Mtei, Tengeru mkoani Arusha, kunapoendelea maandalizi ya maziko ya mwasisi huyo wa Chadema ambaye pia alikuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Golugwa amesema gerezani kuna utaratibu wa katikati ya wiki ambapo mawakili huenda kuonana na Lissu na kuwa wamemtuma Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Wakili Gaston Galubimbi, kwa ajili ya kuchukua ujumbe wa Lissu.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: