Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amekataa kujibu swali aliloulizwa kwenye msiba wa Mzee Edwin Mtei, akieleza kuwa si sahihi kuzungumzia masuala hayo msibani.
Mbowe aliulizwa na mwandishi wa habari kama je, Chadema ya sasa bado inafuata misingi ya muasisi wake, Mzee Mtei?
Mbowe amemuelezea Marehemu Mtei kama mtu aliyejitoa kwa hali na mali kuijenga Chadema na kuwalea kisiasa viongozi wa chama hicho, akiwemo yeye.
Chanzo; Global Publishers