"Pesa hasa kwa sisi wanaume huwa inaamsha ujana, mwisho wa siku mfano unapokwenda baa Saa Saba mchana wale wahudumu wote wanakuwa dada zako.
"Ukishakunywa bia tano wale wahudumu wanageuka hawawi tena dada zako unaona unafaa kuondoka na mmoja wapo. Huwa tunawaambia kwamba wanaonaje wakiifungia pesa sehemu ambayo kuipata sio rahisi?
"Mfano akiwekeza kwenye hati fungani ya UTT AMIS. Ukitaka kuitoa hela yako inakuwa ni siku 10 za kazi kama alikuwa na mbio zake je, huyo Binti ataendelea kumsubiri tu? Hapana!- Charles Ligonja
Chanzo; Clouds Media